Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Basi la Tashrif lililokuwa likitoka Tangakuelekea Dar es salaam, limeungua moto maeneo ya Pongwe karibu na mizaniAjali hiyo imetokea leo Jumanne Septemba 26,2017 saa nane na nusu mchana.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi Benedict Michael Wakuyamba amesema basi hilo lenye namba za usajili T T361 DCF limewaka moto katika eneo la Pongwe jiji Tanga, na hakuna madhara yoyote kwa binadamu zaidi ni hasara ya mizigo ilikuwa imewekwa kwenye buti.Basi hilo liliokuwa likiendeshwa na dereva Hemedi Ali (35) mkazi wa Tanga lilikuwa likitokea Tanga kuelekea jijini Dar es salaam likiwa limebeba abiria 29 lilipofika eneo hilo liliwaka moto.Kamanda Benedict amesema kwamujibu maelezo ya awali ya Dereva huyo anadai alianza kuhisi paipu ya gari inawaka na ndipo aliposimamisha gari hilo.


Post a Comment

 
Top