Usiku
wa August 27 2017 Bondia mwenye sifa ya kutopoteza pambano hata moja
Floyd Mayweather alirudi ulingoni kucheza pambano la 50 dhidi ya Mc
Gregor hiyo ikiwa ni muda umepita toka apigane na Manny Pacquiao na
kumpiga.
Mc
Gregor ambaye alionekana kuwa na tambo alipigwa na Mayweather kwa
Technical Knock Out (TKO)round ya 10 pambano la round 12, huo ukawa ni
mwisho wa tambo zake dhidi ya Mayweather, licha ya kipigo hicho Mc
Gregor kupanda tu ulingoni kulimfanya aingize dola milioni 100 ambazo ni
zaidi ya Tsh bilioni 200 za kitanzania.
Leo
September 10 2017 Mc Gregor anayetokea Ireland ameonekana akiwa amekodi
boti binafsi akiwa na familia yake wanaendelea kula bata Hispania
katika fukwe za Ibiza, kitu ambacho wengi wanaamini anatumia au ana
furaha kuingiza Dola milioni 100 licha ya kupoteza.
Mc Gregor na Mayweather walipopambana






Post a Comment