Gigy Money.
MWANADADA kiwango kwenye Bongo Fleva, Pamela Daffa `Pam D’ amesema
anakerwa na baadhi ya mashabiki wa muziki wanaomshindanisha na
mwanamuziki mwenzake ambaye pia ni muuza sura kwenye video za Kibongo,
Gift Stanford `Gigy Money’ kwamba kushindanishwa huko ni kushushiwa
heshima.
Pam D.
Akipiga stori na Uwazi Showbiz, Pam D anayekimbiza kwenye gemu na Wimbo
wa Ngoma Droo alifunguka kuwa, Gigy kwake ni msanii anayeanza na kamwe
si mwanamuziki wa kumshindanisha naye.
”Mambo ya kushindanishwa na Gigy sipendi, kila mmoja anafanya muziki
wake na ana mashabiki wake, kwanza huyo Gigy hata tukiwekwa naye
jukwaani namfunika, kwa hiyo watu waache kama nilivyo na si
kunishindanisha kusipokuwa na mpango…” alisema Pam D.
STORI: BONIPHACE NGUMIJE | UWAZI
Home
»
»Unlabelled
» GIGY MONEY ,PAM D KIMENUKA LIVE,WATOLEANA MAPOVU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)








Post a Comment