Rais wa Kenya, Uhuru
Kenyatta amezungumza kwa mara ya kwanza tangu Mahakama ya Juu itengue
ushindi wake akisema yuko tayari kurejea kwenye mapambano kuwania
madaraka.Uchaguzi wa marudio unapaswa kufanyika katika kipindi cha siku
60.
Akiwa ameambatana na makamu wake, William Ruto, Kenyatta amesema amekubali uamuzi wa Mahakama licha ya kwamba hauafiki.
Amesema
raia zaidi ya 40 milioni wa Kenya waliamua kukiunga mkono chama chake
cha Jubilee lakini uamuzi wa aliowaita watu sita umebadilisha mambo.
“Hawa
watu sijui watano ...sijui sita wameamua kubadilisha uamuzi uliofanywa
na Wakenya... naomba msife moyo, mimi na mwenzangu tuko tayari kurejea
tena kwenye uchaguzi na tutarudi na ajenda yetu ileile,” amesema
Kenyatta katika hotuba yake kwa Taifa.
Amewataka wananchi wa Kenya kuendelea kuwa wamoja na kutokaribisha tofauti zao, akisema umoja ndiyo nguzo muhimu kwa Wakenya.
“ Naomba tuendelee kuwa wamoja, jirani yako ni ndugu yako,” amesema Kenyatta huku akisisitiza kwa kusema, “amani, amani, amani.
Mahakama
ya Juu imetengua matokeo ya uchaguzi uliofanyika Agosti 8 ambao ulimpa
ushindi Rais Kenyatta kuwa madarakani kwa muhula wa pili.






Post a Comment