Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Msanii wa muziki Bongo na mmiliki wa studio za High Table Sound, Barnaba ameeleza sababu ya baadhi ya nyimbo zake kufanya nje ya studio hiyo.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Mapenzi Jeneza’ amekiambia kipindi cha XXL, Clouds Fm kuwa anafanya hivyo ili kutoa nafasi kwa muziki wake kupata producer mwingine kuusikia.
“Mimi nina studio lakini kukaa kwenye muziki wangu pekee yangu haiwezekani, so ninatoka kwenda kupata masikio mengine, ninawashirikisha ma-producer wengine” amesema Barnaba.
“Kama Mapenzi Jenenza nimejipigia mwenyewe kila kitu, nimeingia studio nime-compose mwenyewe, nimerekodi mwenyewe, nikabeba file nikampa Emma akafanya mixing inasaidia lazima utafute masikio mapya” amesisitiza.
Ameongeza kuwa hajatengeneza studio ili ajifungie mwenye bali ili na wasanii wengine waje wafanye kazi.
 

Post a Comment

 
Top