Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Rapa mkongwe ndani ya tasnia ya bongo fleva, Dudubaya amemtaka msanii mkongwe mwenzake Mr. Nice asiwe kama Kunguru ambaye alikatwa mabawa na watu wengine na kutafuta sababu kuonekana Young D ndiye aliyemkata mabawa hayo.

Dudubaya amesema hayo alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha eNewz kinachorushwa na ting'a namba moja kwa vijana EATV baada ya kusikia kuwa Mr Nice amemlalamikia Young D kuchukua baadhi ya mistari yake ya wimbo wake wa zamani.
Dudubaya amesema kitendo alichofanya Young D kuchukua mistari ya wimbo wake na wimbo wa Mr Nice ni kizuri kwani ameboresha zaidi na kufanya kazi kubwa hivyo uwepo wa kazi hiyo unamfanya hata Mr Nice na yeye kusikika kwenye muziki. 
Aidha Dudubaya alikwenda mbali zaidi na kudai kuwa Mr Nice ameonyesha kulalamika kwa sababu anatafuta sababu ya kutaka kulipwa na Young D kwani amekwama kiuchumi ndiyo maana amelitolea macho jambo hilo.
 

Post a Comment

 
Top