
Silinde ametumia mtandao wake wa Facebook kukanusha taarifa hiyo na kusema kuwa hawezi kufanya usaliti huo kwani anatambua kuwa Ubunge wake huo aliupigania kwa gharama kubwa kwani wapo watu walipoteza maisha, wengine walifungwa huku wengine ndoa zao zikivunjika ili yeye aweze kushinda nafasi ya Ubunge.
Aidha Silinde ametoa ahadi kuwa endapo likitokea jambo hilo basi wananchi waende kuchoma moto nyumba yake na mali zake zote ambazo wanazifahamu kama kuonyesha msisitiza kuwa hawezi kufanya jambo hilo.
"Uzushi unaosambazwa juu yangu katika mtandao wa jamiiforums kuwa nitafanya press kesho ni uongo uliopindukia. Nasema hili likitokea njoo mchome moto nyumba yangu na mali zangu zote mnazozifahamu. Nafasi ya ubunge wa Momba niliutafuta kwa gharama kubwa sana na kuna watu walikufa, wengine walifilisika, wengine wako jela mpaka leo kwa ajili yangu, ndoa zilivunjika n.k siwezi kusaliti kwa maslahi yangu binafsi ya ahadi ya cheo, pesa ama kitu kingine" alisema Silinde
Mbali na hilo Silinde amedai kuwa thamani ya Ubunge haiwezi kushushwa kama vocha ya simu kuwa ikiisha unaweza kukwangua nyingine na kuweka tena






Post a Comment