Rais Dkt. John Magufuli.
RAIS Dkt. John Magufuli amesema Serikali imebaini kuwa kampuni ya Mawasiliano ya Bharti Airtel ni mali ya Shirika la Mawasiliani Tanzania (TTCL) kumwagiza Waziri wa fedha na mipango kufuatilia suala hilo haraka ili Airtel irudishwe kumilikiwa na serikali.
Rais ameyasema hayo leo Desemba 20 wakati akizungumza katika Jengo ambalo litakuwa makao makuu ya Ofisi za Taifa za Takwimu (NBS) mjini Dodoma na sherehe kwenye ya uwekaji jiwe la msingi“Kampuni ya AIRTEL imethibitika kuwa ni mali ya Shirika la TTCL, lakini kuna mchezo ulifanyika, sasa sitaki kuongea sana. Nataka Waziri wa Fedha ufuatilie suala hili kabla ya mwaka huu kuisha,” alisema Magufuli.
Taarifa za ndani zinadai kwamba hisa za Airtel hizo zinatarajiwa kukabidhiwa kwa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na kuendesha biashara za kampuni hiyo yenye wateja wengi zaidi nchini ikiwa nyuma ya Vodacom na Tigo.
Inasemekana TTCL itamiliki hisa zote za Airtel Tanzania Limited ambapo tayari TTCL imewasilisha hoja ya kutaka kufanya hivyo baada ya kubaini kwamba Serikali ilipunjwa kwenye hesabu za uwekezaji.Novemba 3, 1998 ilipoanzisha kampuni tanzu ya Cellnet ambayo ilifanya kazi hadi Mei 7, 2001 ilipobadilishwa jina na kuitwa Celtel Tanzania huku umiliki wake ukiendelea kuwa chini ya shirika hilo kwa asilimia zote baada ya kuwekeza Dola milioni 5 (zaidi ya Sh11 bilioni sasa).Januari 31, 2002, Celtel ikiwa chini ya umiliki wa TTCL ilikopa kiasi cha Dola 82 milioni (zaidi ya Sh180.4 bilioni) ili kukuza mtaji wake. Kwa kipindi hicho, TTCL iliyokuwa na thamani ya Dola 600 milioni (zaidi ya Sh1.32 trilioni) ilikuwa inamilikiwa kwa ubia kati ya Serikali na Kampuni ya Mobile System International (MSI) ya Uholanzi. Serikali ilikuwa inamiliki asilimia 65 ya hisa zote na mbia huyo asilimia 35 zilizosalia.Agosti 5, 2005, mabadiliko yalifanywa kwenye bodi ya wakurugenzi wa Celtel kwa lengo la kuunda kampuni mbili tofauti; Celtel ikitenganishwa na TTCL. Kutokana na mabadiliko hayo, Celtel iliwekwa chini ya umiliki wa MSI ambayo Septemba 2007 iliuza hisa zake kwa Zain ambayo nayo ilikuja kuziuza kwa Bharti Airtel, Juni 8, 2010.

Post a Comment