Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Jacquiline Materu (wa pili kulia) akikabidhi moja ya mashine za kusaidia Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu, Muguha Titus aliyekuwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo, katika hafla ya mapokezi hayo, iliyofanyika katika Hospitali ya Wilaya Kasulu, Mkoani Kigoma Desemba 20, 2017. Wengine pichani ni Muasisi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel (kulia) Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kasulu, Moshi Kigwinya (katikati) pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kasulu, Asia Matitu.


Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Jacquiline Materu akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa tiba kwa ajili ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati kwa Hospitali ya Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma, vilivyotolewa kwa ushirikiano wa Taasisi ya Vodacom Tanzania pamoja na Taasisi ya Doris Mollel.


Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Jacquiline Materu akipokea barua ya shukrani kutoka kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu, Muguha Titus aliyekuwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo, kwa msaada walioutoa kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Doris Mollel pamoja na Vodacom Tanzania. Kulia ni Muasisi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel.​


Post a Comment

 
Top