Mbunge
wa Singida Mashariki kwa tiketi ya (CHADEMA) Tundu Lissu amefunguka na
kuwashukuru Watanzania kwa maombi yao kwake kufuatia oparesheni nyingine ya 19
ambayo amefanyiwa katika mguu wake.
Tundu Lissu jana alifanikiwa kufanyiwa oparesheni hiyo katika
mguu wake wa kulia na kuisha salama, madaktari waliamua kufanya oparesheni hiyo
kufuatia kugundua moja ya mfupa wake ulikuwa ukichelewa kuunga na kudai kuwa
kama wasingefanya upasuaji na kurekebisha mfupa huo ungeweza kuchelewa zaidi na
kuja kuvunjika baadae.
"Ninawashukuru
kwa sala na maombi yenu" aliandika Tundu Lissu kupitia mtandao wake wa
Instagram
Hata hivyo
Watanzania mbalimbali wameendelea kumuombea Tundu Lissu ili aweze kupona haraka
na kurudia tena katika hali yake ya zamani ili aweze kurudi nyumbani Tanzania
na kuendelea na majukumu yake ya kila siku.
Tundu
Lissu alishambuliwa kwa risasi mnano Septemba 7, 2017 na watu wasiojulikana
akiwa mjini Dodoma na kisha baadae kupelekwa nchini Kenya kwa matibabu ambapo
huku alifanyiwa oparesheni kadhaa katika mwili wake na baadae alikwenda nchino
Beljium kwa matibabu zaidi ambapo jana amefanikiwa kufanyiwa oparesheni ya 19.







Post a Comment