Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Leo March 16, 2018 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA  Taifa, Freeman Aikael Mbowe, ameripoti katika kituo kikuu cha Polisi akiwa ameongozana na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Salum Mwalimu ambae alikuwa mgombea katika jimbo la Kinondoni.

Taarifa kutoka kati ukarasa wa Twitter wa CHADEMA inaeleza kuwa Viongozi hao wameachiwa muda huu na wamepangiwa tarehe nyingine nanukuu “Wameachiwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar bila kuhojiwa chochote tangu walipofika kuripoti kituoni hapo asubuhi na wametakiwa kuripoti tena Alhamis,22/3/2018”

Post a Comment

 
Top