Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Msanii wa Bongo fleva  Aslay amesema hajaridhika na mafanikio ambayo ameyapata kupitia mziki wake anaoufanya mpaka atakapo pata tuzo ya heshima  hapa Bongo.

Aslay amesema kwamba pamoja na kufanya nyimbo nyingi hali inayopelekea wasanii wengine pamoja na mashabiki kuhisi kwamba amepata mafanikio makubwa, lakini yeye ataridhika pale atakapopata tuzo mbalimbali ikiwemo tuzo ya heshima.
Hata hivyo Aslay amesema ataendelea na staili yake ya kutoa nyimbo mfululizo huku akieleza jinsi ambavyo anajisikia furaha baada ya kuona wasanii wengine wa Bongo wanaiga staili yake hiyo.
Aidha Aslay ameweka wazi kuwa hapendi kuweka wazi mambo familia yake ndio sababu kubwa inayomfanya 'asimpost' mtoto wake wa pili na sio kwamba anazuiliwa kufanya hivyo na mpenzi wake wa sasa (Tessychocolate) kama inavyoelezwa mitandaoni.
 

Post a Comment

 
Top