Hosptali
ya Taifa Muhimbili MNH imetakiwa kuwa mfano bora wa kuigwa katika kupambana na
rushwa kwa kusimamia haki ya mteja, kutimiza wajibu wa mtoa huduma, maadili ya
taaluma na kutekeleza misingi ya utawala bora.
Hilo limesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya
Hosptali hiyo, Dk Hellen Kondya wakati akizindua rasmi kamati ya uratibu na
kamati ya kudhibiti uadilifu wa hospitali hiyo.
Dk. Kondya
amesema ni muhimu kuweka, uhusiano kati ya majukumu ya kamati hizo na maadili
ya kitaaluma ambayo yamebainishwa vyema katika sheria mbalimbali za taaluma za
sekta ya afya.
Naye Mkurugenzi
mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru amesema Hosptali hiyo imeunda
kamati hizo ikiwa ni mwitikio wa utaratibu wa serikali unaozitaka idara za
serikali na taasisi za umma kusimamia na kudhibiti uadilifu.







Post a Comment