Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Jeshi la polisi mkoani Kagera linamshikilia Mwalimu Deogratius Saimon mwenye miaka 34 ambaye ni mwalimu wa shule ya Sekondary Nyakisasa iliyopo mkoani Kagera kwa kosa la kutoa lugha ya matusi kwa Rais wa Tanzania Dr. John Magufuli.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Augustine Ollom amesema kuwa mwalimu huyo anashikiliwa kwa kosa la kutumia ukurasa wake wa Facebook kuikashfu serikali na kumkashfu Rais Magufuli  kuwa ni Dikteta na anaminya demokrasia.
Aidha amesema kuwa kufutia hali hiyo tayari yupo mikononi mwa polisi na watakwenda naye mpaka dakika ya mwisho ili sheria iweze kutenda haki huku Kamanda amewaomba wananchi kuendelea kufichua watu wenye vitendo vya namna hiyo ili wawakabidhi polisi ili washughulikiwe

Post a Comment

 
Top