Naibu
Katibu Mkuu wa BAVICHA, Getrude Ndibalema amefunguka na kusema kuwa ameamua
kujiuzulu nafasi yake hiyo katika chama cha CHADEMA na kubaki mwanachama wa
kawaida ili aweze kujikita zaidi katika fani yake.
amesema kuwa ametafakari sana na kuamua kufanya maamuzzi hayo
ili aweze kujikita kwenye shughuli zake nje ya siasa na kudai barua ambayo
imesambazwa kwenye mitandao ya kijamii ni kweli ameiandika yeye ili umma uweze
kutambua hilo.
"Nimekuwa
Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) Tanzania bara
toka mwaka 2014 mpaka mwaka Machi 11, 2018 na barua ambayo imesambaa kwenye
mitandao ya kijamii ni ya kwangu na ni rasmi kabisa imetoka kwangu na niliituma
usiku kuamkia tarehe 12 na lengo la kuandika barua ile ni kuwapa taarifa Umma
pamoja na wanachama wa CHADEMA pamoja na wapenzi wa CHADEMA kwamba nimejivua
nafasi yangu ambayo ni nafasi ya kitaifa na kubakia mwanachama wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo yaani mtanzania wa kawaida kabisa na mwanachama wa
kawaida"
Aidha Ndibalema
ameweka wazi sababu kubwa yeye kufanya maamuzi hayo
"Nimetafakari
sana na nimeamua kujikita katika shughuli zangu binafsi hasa zinazohusiana na
taaluma yangu ya mawasiliano kwa Umma, nimesoma Masters ya Mass Communication kwa
hiyo nataka nishughulike na mambo hayo sasa" alisisitiza
Ndibalema







Post a Comment