Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
MSANII wa Bongo Fleva aliyepata kutamba na ngoma zake kali zikiwemo Kinyulinyuli na Ukipenda, Samir Kassim amezinduka usingizini baada ya kupotea kwa kipindi kirefu na kusababisha mashabiki wake kuhoji alikopotelea.


Samir alifunguka kuwa, alipototea kidogo kutokana na mambo ya kimaisha, lakini sasa amerejea upya ukiwa akiwa na zawadi spesho kwa ajili ya mashabiki wake.

“Sasa nimerejea, nina zawadi nzuri kwa mashabiki wangu ambayo ni ngoma mpya ambayo nimeachia inayokwenda kwa jina la Sawa. Ninaamini kabisa kila mmoja ataipenda na kuvutiwa nayo na pia sitalala tena,” alisema Samir.

Post a Comment

 
Top