Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, amesema kuwa, baada ya miezi mitatu Serikali itatoa uamuzi kama nchi iendelee kutumia mita za umeme zinazotengenezwa nje ya nchi au kupiga marufuku uingizaji wa mita hizo.

Dkt. Kalemani ameyasema hayo jijini Dar es Salam wakati alipofanya ziara katika kiwanda cha Baobab Energy Systems kinachozalisha mita za umeme lengo likiwa ni kujiridhisha na uwezo wa kiwanda hicho katika kukidhi mahitaji ya mita nchini.
"Serikali imeweka miezi mitatu ya matazamio ili kuona kama viwanda  vyetu ambavyo sasa ni viwili, vina uwezo wa kuzalisha mita za umeme  za kutosha na zenye ubora zitakazokidhi soko la ndani, kisha tutatoa uamuzi kuhusu uingizaji wa mita hizo nchini," alisema Dkt. Kalemani.
Aidha Waziri Kalemani ameongeza kuwa, uzalishaji wa vifaa vya umeme nchini una faida mbalimbali ikiwemo kupungua kwa gharama za usafirishaji, mita kupatikana kwa haraka, kwa gharama nafuu na kwa wingi.
"Mita moja ya njia moja ya umeme (single phase) kutoka nje ya nchi ni shilingi 150,000 na njia Tatu za umeme (three phase) ni mpaka shilingi Laki Saba, lakini mita zinazozalishwa nchini unazipata si kwa zaidi ya shilingi 120,000 kwa mita za njia moja ya umeme na haizidi shilingi  Laki Nne na Nusu kwa mita za njia Tatu za umeme," alisema.
Kwa upande wake  Mkurugenzi wa kiwanda hicho cha Baobab, Hashim Ibrahim, alimweleza Dkt Kalemani  kuwa kiwanda hicho kina unawezo wa kuzalisha mita 38,000 kwa mwezi na kwa mwaka wanazalisha mita 456,000.
 

Post a Comment

 
Top