Msanii
wa muziki bongo ambaye kwa sasa mjasiriamali anayehakikisha matumbo ya watu
yanapata afya, Shilole au Shishi Trump, hatimaye amefunguka kuhusu kuvunjika
kwa ndoa yake na mume wake Uchebe.
Shilole amesema hajaachana na mume wake na wala hawafikirii
kuachana.
Kwa upande wa
mume wake Shilole Bwana Uchebe amesema sio kweli kwamba ameachana na mkewe, na
kwamba kuna wanafiki wanapenda wasikie wameachana.
Akifunguka
kuhusu kupost kwa ua jeusi na caption yenye utata, Uchebe amesema kuna mtu
alihack acount yake na kupost hivyo, lakini hawajaachana namkewe na wala sio
kiki.
“Sio kweli
sijaachana na mke wangu na wala hatufikirii kuachana, kuna watu wanafiki
wanapenda kusikia tumeachana, kuhusu ile post kuna mtu alifanikiwa kuhack
acount yangu na kupost vile lakini sijamuacha mke wangu, na wala hatuna ugomvi,
na niwaambie tu kuwa hatuachani leo hata kiama”, amesema Uchebe.
Tetesi za
wawili hao kuachana zimekuja baada ya kupostiwa kwa ua jeusi kwenye ukurasa wa
instagram wa Uchebe na caption ambayo ilikuwa na utata, na watu kuhisi labda
wawili hao hawako pamoja tena.







Post a Comment