Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dkt. Mwigulu Nchemba amezungumzia maiti zinazookotwa baharini na kusema kuwa kama zingekuwa za Watanzania basi sauti za familia zao zingekuwa kubwa sana.


Akaongeza kuwa maiti hizo huokotwa katika fukwe za bahari ya Hindi ambayo Tanzania inachangia na mataifa mengi hivyo zinaweza kuwa zimesafiri kwa upepo kutoka mbali.

Kuna baadhi ya watu wanaosafirishwa kupitia Tanzania kwenda mataifa mengine ambao husafirishwa katika mazingira hatarishi na ikitokea wamefariki basi hutupwa na watu wakiona badala ya kuhoji wanaishia kusema watu wanauawa.

Waziri Mwigulu amesema kuwa mpaka sasa hakuna tishio la kuuawa kwa watu nchini na kusisitiza watu kutoa taarifa pale wanapohofia usalama wao.

Post a Comment

 
Top