Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

 Vincent Kigosi ‘Ray’ amemwaga sifa nyingi kwa mzazi mwenziye, Chuchu Hans, kwa kusema kuwa ni mama bora anayejua kumlea vziuri mtoto wao, Jaden.

Ray alisema kuwa, Chuchu amekuwa ni mstari wa mbele katika kuhakikisha mtoto wao anakuwa na afya njema na pia anakuwa kwenye mazingira mazuri siku zote.
“Unajua angekuwa mwanamke mwingine, angeona mtoto anamzibia vitu vingi hasa kwenye upande wa kuendelea kucheza filamu, lakini aliweka pembeni lengo likawa moja tu, kumuangalia mtoto tu,” alisema Ray.

Muigizaji huyo aliongeza kuwa, anamuombea sana kwa Mungu mzazi mwenziye huyo aendelee kuwa na moyo huo wa malezi bora kwa mwanaye kwani mama ndiye hubeba kwa asilimia kubwa jukumu la malezi.

Post a Comment

 
Top