Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amefunguka na kuitaka jamii kiujumla kuacha kukata tamaa katika kupigania kufikia malengo yao ambayo wameyapanga kuyafanya au wanayoyafanya kwa sasa


Dkt. Kigwangalla ametoa ushauri huo kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii baada ya kuwepo ya tabia ya baadhi ya watu kupenda kukatisha tamaa wenzao katika mambo wanayofanya ili wasifanikiwe kimaisha au kumzidi yeye.
"Komaa na ndoto yako usikate tamaa, kamatilia kamba ya mikakati yako mpaka uvuke usiachie. Mto wa maisha unatiririka na ndani yake kuna Mamba, Viboko na miamba, ukiachia kamba hujui utaangukia kwenye nini usiachie komaaa, pambana, songa mbele uvuke vikwazo", amesema Kigwangalla.
Kwa upande mwingine,Dkt. Kigwangalla amesema kuwepo na maisha bila ya ndoto ni sawa na shamba la mahindi lililogeuka kuwa jeruba la mpunga kwa kuvamiwa na mafuriko.

Post a Comment

 
Top