Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu amepiga marufuku utoaji wa mikopo midogo midogo kwa wanawake kwa madai haitoweza kuwasaidia katika juhudi za kuwakwamua kiuchumi.

Waziri Ummy ametoa kauli hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani yaliyofanyikia mkoani Songwe na kuwapa miezi mitatu Wakurugenzi wote nchini kuhakikisha wanatenga asilimia nne za fedha za halmashauri kwa ajili ya kuwapa wanawake mikopo ili waweze kujiendelea kimaendeleo na kuunga  mkono juhudi za serikali katika uchumi wa viwanda.

"Masuala ya kuwapa wanawake mikopo watu sita laki tatu yamepitwa na wakati maana sijui itawasaidia kitu gani ?, kwa hiyo napiga marufuku suala la watu kupewa laki tatu, watafanya shughuli gani ambayo itahusiana na masuala ya maendeleo ya viwanda huu ni upuuzi", amesema Ummy.

Post a Comment

 
Top