Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani(mwenye miwani) na Mbunge wa Urambo Magreth Sitta na viongozi wengine wakikata utepe wa uzinduzi wa uwashaji wa umeme wa REA katika Kijiji cha Jionee Mwenyewe kata ya Songambele jana.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akibonyesha kitufe kuwasha umeme katika Kijiji cha Jionee Mwenyewe Kata ya Songambele baada ya kukamilika kwa mradi wa uwekaji wa miundombinu katika eneo hilo.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani(mwenye miwani) na Mbunge wa Urambo Magreth Sitta(kushoto) na wananchi wa kiijiji cha Jionee Mwenyewe kata ya Songambele wakishangilia mara baada ya uzinduzi wa uwashaji wa umeme katika eneo hilo jana.
Waziri wa Nishati Medard Kalemani akimpongeza Diwani wa Kata ya Vumilia kupitia ACT Wazalendo Kassim Shushu (kushoto) baada ya kumkabidhi eneo la shamba lake linalokadiriwa kuwa ekari moja kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Kupozea umeme. Picha na Tiganya Vincent
SERIKALI
imesema ni marufuku kwa Wakandarasi na Wataalamu kuruka nyumba wakati
wa uunganishaji wa umeme kwa wananchi kupitia Mradi kabambe wa
kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatuunatekelezwa na Wakala wa Umeme
Vijijini (REA).
Kauli
hiyo ilitolewa jana wilayani Urambo na Kaliua na Waziri wa Dkt. Medard
Kalemani wakati alipokuwa akigaua utekelezaji wa zoezi la usambazaji wa
umeme wa REA katika maeneo hayo.
Alisema
ni marufuku kuruka nyumba hata kama ni nyasi kama mwananchi anataka
umeme na amelipa shilingi 27,000 za kuunganishiwa umeme.
Kalemani
alisema kuwa mpango wa Serikali ni kuhakikisha umeme unafika katika
vijiji na vitongoji vyote na kwa wananchi wote bila kubagua.
“Nawaagiza
Wakandarasi na Wataalamu wote hakuna kuruka nyumba wala kubagua nyumba
kwa sababu ya kuwa imeezekwa kwa nyasi…umeme ni nyumba kwa nyuma , kaya
kwa kaya.., hata kama mtu hajakamisha nyumba yake kama kuna mti karibu
na nyumba yake wekeeni hata hapo ili iwe rahisi kuingiza umeme
atakapokuwa amekamisha nyumba yake” alisisitiza Waziri huyo.
Alisisitiza
kuna mtindo wa Wakandarasi kuchagua nyumba wakati wanapotekekeza
majukumu yao ya kuwaweka umeme , na kusema kuwa kwa hivi sasa hilo ni
marufku umeme ni kwa wote wanaotaka.
Waziri
huyo wa Nishati aliongeza kuwa ni marufuku kuwatoza wananchi wanaotaka
kuunganishiwa umeme zaidi ya shilingi 27,000/- na kutoa wito kwa
mwananchi atayetozwa zaidi ya kiasi hicho atoe taarifa ili hatua kali
dhidi ya wahusika ziweze kuchukiwa.
Aidha
alitoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa hiyo ya kuunganishiwa kwa
gharama hizo kwani baada ya hapo itabidi walipie kulingana na taratibu
za Shirilka la Ugavi wa umeme Tanzania(TANESCO)
Katika
hatua nyingine Waziri huyo wa Nishati amemupongeza Diwani wa Kata ya
Vumilia Wilayani Urambo Kassim Shushu kwa kutoa eneo lake kwa ajili ya
kuwapatia TANESCO ili wajenge kituo cha kupozea umeme.
Alisema
kitendo hicho cha Diwani wa Kata ya Vumilia kupitia ACT Wazalendo ni
cha kizalendo na kimeonyesha kuwa maendeleo hayana chama na baada ya
kukamilisha mradi TANESCO itabidi waone jinsi ya kumpa mkono wa
shukurani.
Dkt
. Kalemani alisema baada ya Shirika lake la la Ugavi wa Umeme
Tanzania(TANESCO) litajenga Kituo kidogo cha kupozea umeme (sub station)
katika Kijiji hicho cha Uhuru ili kuboresha upatikanaji wa huduma ya
umeme kwa wananchi wa Wilaya ya Kaliua na Urambo na maeneo jirani.
Alisema
Kituo kikingine kitajengwa mpakani mwa Tabora na Kigoma kwa ajili ya
kuuwezesha na Mkoa wa Kigoma kuwa na umeme wa uhakika.










Post a Comment