Aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, George Lwandamina ameungana na
timu yake hiyo ya zamani kwa kuandika ujumbe unaoitaka kuhakikisha
inachomoza na ushindi dhidi ya wapinzani wao Welayta Dicha kwenye mchezo
wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika unaotarajiwa kupigwa hii leo
majira ya saa 10:00 alasiri.
Katika kuonyesha mapenzi yake kwa wanajangwani hao na bado yupo pamoja nao, Lwandamina ameamua kuungana na Yanga SC kwenye kipindi hiki kwa kuandika ujumbe huo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Facebook.
Ushindi ni fikra inayofurahisha nafsi ya kila kitu. Kila lakheri vijana.
Lwandamina ameandika maneno hayo ambayo yatakayo leta faraja kwa mashabiki na wachezaji wa Yanga SC na hamasa wakati wakiwa wanakabiliwa na mechi dhidi ya Welayta Dicha michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.






Post a Comment