Mbunge wa Jimbo la Kawe (CHADEMA), Halima Mdee ameendeleza hoja kuhusu matumizi ya fedha ambazo hazijulikani zimetumikaje, kama ilivyobainishwa kwenye ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
Kupitia akaunti yake katika Mtandao wa JamiiForums, Mdee amemtaka Rais Magufuli na Serikali kwa ujumla kuacha kutumia vitisho na badala yake wajikite kwenye kutoa majibu sahihi kuhusiana na matumizi ya fedha hizo, ili kuondoa mkanganyiko uliopo kwa wananchi
Aidha, Mbunge huyo amehoji masuala mengine 8 yenye utata yaliyomo kwenye Ripoti hiyo ya CAG na kuwataka wananchi waamke kutoka kwenye usingizi wa pono unaoligharimu Taifa
Mwisho, Halima Mdee amemueleza Rais Magufuli kupitia hayo mambo 8, ajipime kama amefanikiwa kuinyoosha nchi au nchi imemnyoosha






Post a Comment