Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 Arsenal boss Arsene Wenger announced the shock decision to step down at end of the season
 Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger sasa ametangaza rasmi kung’atuka ndani ya timu hiyo kama kocha baada ya kuiongoza kwa miaka 22.

Wenger mwenye umri wa miaka 68 amejiunga na Arsenal akitokea Nagoya Grampus Eight mwaka 1996, ameandika ujumbe wenye hisia kubwa kwa klabu na mashabiki wa timu hiyo akitangaza adhima yake ya kuondoka.
Meneja huyo raia wa Ufaransa ameuwambia mtandao wa klabu hiyo kuwa baada ya kutafakari kwamakini ameamua kuachia nafasi yake ya kocha mwishoni mwa msimu huu.
Baada ya kutafakari kwa makini na mazungumzo yangu na uongozi wa klabu nadhani nimuda muafaka sasa wa mimi kujiudhuru nafasi yangu mwishoni mwa msimu.
Ninashukuru kwa kupata nafasi ya kuihudumia timu hii kwa miaka mingi, nimeiyongoza timu hii kwa moyo wangu wote.
Kwa wapenzi wote wa Arsenal kuweni makini na thamani ya timu hii. Upendo wangu na mchango wangu utakuwepo daima.

Post a Comment

 
Top