Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Msanii wa muziki kutoka Visiwani Zanzibar, Baby J amefunguka kuwa hana mpinzani katika muziki anaoufanya.
Baby ameeleza kuwa hajawahi kuwa na mpinzani katika muziki anaofanya yeye, Licha ya kuwa miaka ya zamani alikuwa akishindanishwa na mwanamuziki Sainaj kutokea huko huko, mrembo huyo amekana kuwa na mpinzani.
“Kwanza sijawahi kuwa na mpinzani, kwa sababu siku zote unakuwa unajiona wewe mwenyewe huoni cha mbali mimi navyo jiona yani kwanza nime zaliwa Zanzibar, nimefumbua macho Zanzibar, hao wote wanaojiita wapinzani ndiyo nimewepokea hapa Zanzibar, so siamini kama nina mpinzani,” amesema mrembo huyo ambaye hivi karibuni ameshirikishwa kwenye ngoma mpya ya Kasssim Mganga.
Pia ameongeza kuwa moja ya sababu zinazowafanya wasanii wa kike kuwa wa chache kisiwani humo ni kutokana na kutokujiamini.

Post a Comment

 
Top