Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akisalimiana na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro (ACP) Hamisi Issah, na anayeshuhudia katikati ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha (DCP) Charles Mkumbo, alipowasili mkoani Arusha, kuwapa pole askari wa jeshi hilo kufuatia ajali ya moto iliyoteketeza makazi yao waliyokuwa wakiishi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiangalia eneo lililoathiriwa na ajali ya moto iliyoteketeza makazi ya askari tukio lililotokea jana majira ya jioni, IGP Sirro yupo mkoani Arusha, kwa ajili ya kuwapa pole askari na familia zao pamoja na salamu za pole kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli, na kutoa jumla ya kiasi cha shilingi milioni 260 kwa ajili ya kujenga upya makazi yao kulia ni kamanda wa Polisi mkoani humo (DCP) Charles Mkumbo

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (kulia), akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, alipowasili mkoani humo kwa ajili ya kuwapa pole askari na familia zao kufuatia ajali ya moto iliyoteketeza makazi yao waliyokuwa wakiishi pamoja na kuwapa salamu za pole kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli, na kutoa jumla ya kiasi cha shilingi milioni 260 kwa ajili ya kujenga upya makazi yao. Picha na Jeshi la Polisi.

Post a Comment

 
Top