
Alikiba.
MUZIKI
Bongo upo katika utamu na una ladha ya aina yake kutokana na ushindani
uliyopo kwa sasa. Yaani wakati soko la muvi likiendelea kudorora, muziki
umezidi kukua na kwa sasa ushindani umehamia kwenye mtandao wa YouTube,
wanamuziki wakitunishiana misuli kuwa nani anapata ‘views’ wengi katika
mtandao huo.Kwa sasa haijarishi wimbo wako mtaani unaimbwa ama
unasikika kwa kiasi gani. Video umefanyiwa Sauz au Mwananyamala mitaa ya
Makoroboi hapa Bongo, watu wapo kwenye namba, YouTube wimbonasomaje na
umetazamwa na watu wangapi?

Roma Mkatoliki.
Hilo
ndilo la msingi kwa sasa. Ndiyo maana ingawa wimbo wa Aslay uitwao
Pusha unafanya vizuri mtaani lakini kwenye mitandao siyo gumzo maana
hana namba YouTube, hata kwenye kumi bora za wanamuziki wanaokimbiza
Bongo hayumo!Ndicho kilichomkuta Nay wa Mitego na wimbo wake uitwao
Makuzi, hapa chini Uwazi Showbiz inakuletea wakali kumi wanaokimbiza kwa
sasa Bongo kwenye mtandao wa YouTube.

Nay wa Mitego.
Ali
Kiba- Seduce Me Huyu ndiye kinara wa YouTube kwa sasa Bongo. Wimbo wake
wa Seduce Me mpaka gazeti hili linaingia mitamboni siku ya Jumapili
jioni ulikuwa umetazamwa na watu wanaozidi milioni 3. 7 huku wimbo wa
msanii mwingine wa Bongo Fleva uitwao Zilipendwa umetazamwa na zaidi ya
watu milioni 2.9.
R.O.M.A-
Zimbabwe Wimbo wa Zimbabwe wa Roma uliofanywa na Produza Joff Master wa
Tongwe Records ndiyo unafuata ukishika namba tatu na umetazamwa na watu
wanaozidi milioni 1. 3.

Vee Money.
Vee
Money- Kisela Vee Money ni mwanamuziki wa kike pekee ambaye anaingia
kwenye kumi bora za wanamuziki Bongo wanaokimbiza YouTube. Wimbo wake wa
Kisela aliomshirikisha Mr. P kutoka Kundi la P Square unashika namba
nne na umetazamwa na watu wanaozidi milioni 1.2.

Jux.
Jux-
Utaniua Wimbo huu hauna muda kwenye mtandao huo wa YouTube. Lakini
umeweza kufanya vizuri na kuzizidi nyimbo nyingi ambazo zimetoka kabla
yake. Unashika namba tano na umetazamwa na watu wanaozidi laki 7. 5.
Hawa
nao wamo! Namba sita inashikwa na Joh Makini ft. Davido wimbo Kata Leta
ambao umetazamwa na watu wanaozidi laki 6.4 huku Chege na wimbo wake wa
Runtown ukitazamwa na watu wanaozidi laki 4.2.

Joh Makini.
R.O.M.A
narudi tena kwenye listi hii safari hii akiwa na Stamina na project yao
ya iitwayo Rostam ambapo wamefanya wimbo uitwo Hivi ama Vile. Wimbo huu
umetazamwa pia na watu wanaozidi laki 4.2.
Bill
Nass anachukua nafasi ta tisa na Wimbo wa Sina Jambo. Wimbo huu
umetazamwa na watu laki 3. 8 huku Fid Q akifunga mkia na wimbo wake
uitwao Fresh ambao
umetazamwa na watu laki 2. 5. Data hizi ni kabla ya jana Jumatatu!






Post a Comment