Mnada
wa nyumba ya pili za mfanyabiashara maarufu Said Lugumu, zilizopo
maeneo ya Upanga jijini Dar es Salaam umeahirishwa Ijumaa hii.
Mnada huo ambao umekuwa ukisimamiwa na kampuni ya Yono, umeahirishwa kutokana na sababu za wateja ambao walitaka kununua nyumba hiyo kushindwa kufika bei ambayo ilitakiwa kuuzwa.
Wateja ambao walitakiwa kununua nyumba hiyo walikwama kwenye bei ya shilingi milioni 650.
Wakati huo huo katika nyumba ya kwanza iliyopo katika eneo la Mbweni JKT ilishindwa kununuliwa kutokana na tatizo kama hilo baada ya wanunuzi wa mwisho walikwama kwenye bei ya shilingi milioni 510.






Post a Comment