Rais mpya wa Zimbabwe, Mh. Emmerson Mnangagwa ameapishwa leo mchana kwenye uwanja wa michezo wa Harare nchini Zimbabwe.
Rais mpya wa Zimbabwe, Mh. Emmerson Mnangagwa na mkewe Auxillia wakiwasili uwanjani kabla ya kuapishwa leo mchana.
Rais mpya wa Zimbabwe, Mh. Emmerson Mnangagwa ameapishwa leo mchana huu na hivyo kuhitimisha miaka 37 ya utawala wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Mh. Robert Mugabe aliyetangaza kujiuzulu tangu Jumanne iliyopita.
Mamia ya wananchi wa Zimbabwe wamefurika katika uwanja wa Michezo wa Harare kushuhudia sherehe hizo ambazo pia zimehudhuriwa na marais Philipe Nyusi wa Msumbiji, Edger Lungu wa Zambia , Luteni Jenerali Dkt. Seretse Khama Ian Khama, Joseph Kabila wa DRC na Marais wastaafu Hifikepunye Pohamba wa Namibia, Dkt. Keneth Kaunda wa Zambia, Sam Nujoma wa Namibia na viongozi kutoka mataifa mbalimbali ya maziwa makuu na wa mataifa matatu.
Kelele, vivijo na nderemo vimesikika wakati Mnangagwa akikamilisha kiapo chake. Mitaani kumekuwa na hali ya shamra shamra za tukio hilo lililokuwa likisubiriwa na wengi huku akkagua gwaride la heshima na kupigiwa mizinga 21 kama Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi wa ulinzi na Usalama wa taifa la Zimbabwe.
Baada ya Kiapo hicho Rais Emmerson Mnangagwa aliwaapisha wakuu wa vyombo vya ulinzi na kusalimiana nao.






Post a Comment