Nyumba ya Lugumi iliyoko JKT Mbweni ambayo leo imeshindikana kuuzika baada ya waliotaka kuinunua kukomea kiwango cha Sh. milioni 510, hivyo kutofikia kiwango kilichotakiwa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) na kusababisha mnada mwingine kuitishwa tarehe itakayotajwa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mnada ya Yono, Scolastica Kevela (kulia) akiwa eneo la mnada Mbweni leo. Kushoto ni mwandishi wa habari wa Global TV Online, Felista Masae.
NYUMBA ya Lugumi ya JKT Mbweni jijini Dar es Salaam imeshindikana kuuzika kwa mara ya pili kutokana na waliotaka kuinunua kukomea Sh. Milioni 510, hivyo kushindwa kufikia kiwango kinachotakiwa na Mamlaka ya Kodi nchini (TRA).
Nyumba hiyo ilishindikana kuuzika katika mnada uliopita baada ya aliyependekeza kuinunua, Dtk. Louis Shika maarufu kama “Mzee wa 900 Itapendeza” kushindwa kutoa fedha ya awali ambayo ni asilimia 25 na hivyo kuishia mikononi mwa polisi.
Mnada huo umeahirishwa tena hadi tarehe itakayotajwa.








Post a Comment