Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Wakiwasili katika kaburi la Kanumba.
NGULI wa filamu za Nigeria, Ramsey Noah amesema japokuwa miaka mingi imepita tangu kufariki dunia kwa aliyekuwa msanii mahiri wa filamu za Kibongo, Steven Kanumba, bado pengo lake haliwezi kuzibika katika ulimwengu wa tasnia ya filamu.


Wakiweka maua katika kaburi hilo.

Akizungumza katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam alikoenda kuzuru kaburi la marehemu Steven Kanumba leo Jumamosi, Desemba 16, 2017, Ramsey, alisema Kanumba aliondoka kipindi ambacho nyota yake ya mafanikio ndiyo kwanza ilikuwa imeanza kung’ara na kwamba, kila anapomkumbuka na mambo waliyoyafanya pamoja, huwa haamini kama hatamuona tena maishani mwake.

Mama Kanumba akiangua kilio kifuani mwa Ramsey.

Ramsey alizuru hapa nchini kuhudhuria Tamasha la Kutambua Fursa kwa vijana lilioandaliwa chini ya Kampuni ya Sahara, tamasha hilo lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), juzi Alhamisi.

Katika kuzuru kaburi hilo  aliongozana na mama mzazi wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa, mdogo wa marehemu, Seth Bosco, wasanii wa filamu na mashabiki wa marehemu Kanumba.
Ramsey akizungumza na wanahabri makaburini hapo.

Ramsey ndiye msanii wa kwanza mkubwa nchini Nigeria kufanya filamu na Mtanzania ambapo walifanya Moses na Devil’s Kingdom jambo ambalo liliunganisha Bongo Movie na Nollywood hivyo kutengeneza uhusiano imara kati ya nchi hizi mbili katika tasnia ya filamu.

Post a Comment

 
Top