Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ akiwa na mpenzi wake.
MKONGWE wa Muziki wa Afro Pop Afrika Mashariki, Judith Wambura Mbibo
‘Lady Jaydee’ anamaliza mwaka kwa kuachia video ya kibao chake kipya na
cha kwanza kufanya na Taurus Musik, Baby.
Jide amesaini mkataba na lebo hiyo ya Kenya kwa miaka mitatu, ambayo
ndani yake, atatengeneza albamu mbili, ikiwemo pia albamu yake ya kwanza
ya video. Katika video yake mpya, mwanamuziki huyo amemshirikisha
mpenzi wake, Spicy ambaye ni raia wa Nigeria. Hii ni video ya pili
kucheza pamoja na Spicy ambaye pia ni mwanamuziki, ya kwanza ikiwa ile
ya ngoma yao waliyofanya pamoja, Together Remix.
“Ni mkataba mzuri kwangu kwa sababu umezingatia masilahi ya pande
zote mbili, ile lebo pia ni kubwa hapa Afrika Mashariki, wanafahamu nini
cha kufanya ili msanii atimize malengo yao na yake pia, kwa hiyo ni
suala la kujivunia,” anasema Jaydee katika mazungumzo kupitia mtandao wa
WhatsApp. “Nimemshirikisha Spicy kwa sababu anafit kwenye nafasi ile,
ni msanii lakini kumbuka pia ni mwenza wangu, nadhani nitafanya video
nyingi pamoja naye, hata kumi ikibidi, kwani kuna ubaya wowote?”







Post a Comment