Mwanamitindo Hamisa Mobeto.
Mwanamitindo Hamisa Mobeto anadaiwa kunasa mtegoni baada ya ‘kuuvaa
mkenge’ ulioratibiwa na hasimu wake wa siku za hivi karibuni, Zarinah
Hassan ‘Zari’.
Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na Zari, inadaiwa kuwa
mjasiriamali huyo alimtumia mtu aitwaye William Bugeme ambaye pia ana
ukaribu naye wa damu, ili aweze kumchukua mwanamitindo huyo, ambaye
amezaa na baba wa watoto wake wawili.
Inadaiwa lengo la Zari ni kuona wawili hao wakiwa karibu, basi ni
dhahiri kuwa ukaribu kati ya Hamisa na baba watoto wake utaisha, kwani
uhusiano wa kimapenzi na William hauwezi kukubalika.
“Mnajua kuwa huyo Hamisa amenasa kwa Bugeme lakini hajui kuwa huo ni
mpango wa Zari ili amtoe kwa baba mtoto wake, asipoangalia atatumika tu
kisha atabwagwa kwani jamaa yupo kimaslahi zaidi kwa ajili ya kuokoa
penzi la dada yake,” alisema Sosi huyo.
Kwa mujibu wa sosi huyo, picha za wawili hao wakiwa katika pozi tofauti zilinaswa hivi karibuni zikiwa zimerushwa mtandaoni.
Zarinah Hassan ‘Zari’.
Sosi huyo alikwenda mbali zaidi na kuvujisha siri ya Zari kuwa ndiye
anayemtuma ndugu yake huyo ili akifanikisha kuwa naye kimapenzi itakuwa
rahisi kuachana na baba wa watoto wake.
Hata hivyo sosi huyo alidai fungu kubwa na zuri limeandaliwa kuhakikisha Hamisa hakwepi mtego huo.
“Mwanamke ni mjanja sana sana haongei ni pesa ndio inaongea, Bugeme
toka zamani anafahamiana na Hamisa sasa ameamua kumtumia huyo huyo ili
kuumaliza mchezo wake kabisa, unadhani mzazi mwenzake akiona ameingia
kwenye penzi na Bugeme ataendelea naye, amecheza kwelikweli








Post a Comment