Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Msanii wa muziki wa bongo fleva Nandy, amesema anamshukuru Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa pongezi alizompa, kwani ni kitu ambacho hakikutarajia.

Nandy amesema kuwa ni kitu cha faraja kuona anapongezwa na kiongozi mkubwa serikalini, hivyo kimempa faraja.

“Nimefurahi kwa sababu ni mtu ambaye ananisapoti sana, na imenipa faraja sana kwani sikutarajia, kwa sababu mi nilitumiwa kwenye group nikaiona, basi nikampigia simu nikaongea naye nikamshukuru”, amesema Nandy.
Naibu Spika Tulia Ackson amepost kwenye instagram yake akimpongeza Nandy kwa jitihada zake anazozifanya kwenye kazi yake ya sana ya muziki.

Post a Comment

 
Top