Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Muimbaji nguli wa muziki wa dance nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ amesema hana mpango wa kufanya show zaidi ya kuwa msanii wa studio.


Muimbaji huyo aliyejizolea umaarufu na ngoma ‘Seya’ ameiambia Leo Tena ya Clouds kuwa mwanae, Papii Kocha ndiye atakuwa anafanya show zaidi.
“Nitafanya show kwa kuwashukuru Watanzania wote, baada ya hapo nitakuwa msanii wa studio, kofia yangu nitamuachia mwanangu Papii,” amesema Babu Seya.
Wawili hao walikuwa wakitumikia kifungo jela walipewa msamaha na Rais John Magufuli kwenye maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru. Tangu kuwa uraiani Papii Kocha ametoa wimbo mmoja uitwao Waambie.

Post a Comment

 
Top