Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

 Msanii Chid Benz amesema taarifa za yeye kuuza nyumba yake ya ghorofa ni za kweli.

Rapper huyo ameiambia E-Newz ya EATV licha ya kuuza nyumba hiyo bado anaendelea kuuza nyumba alizonazo ila kwa sasa anaishi kwa mama yake.
“Nimeuza nyumba ghorofa, na sio ya kwanza kuiuza, nimeuza nyumba nyingi na sasa ninaishi kwa Mama yangu mzazi ambayo ni nyumba nimejenga mimi,” amesema.
“Nimeuza ghorofa na nimeuza nyumba nyingi ambazo nazimiliki na ninaendelea kuuza nyumba pia,” ameongeza.
January mwaka huu Jeshi la Polisi mkoani Dodoma lilimshikilia Chid Benz kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya, hiyo ilikuwa ni mara ya tatu kwa msanii huyu kukumbwa na sakata kama hilo.

Post a Comment

 
Top