Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
PATI ya bethidei ya dada wa staa wa Afro-Pop, Ali Kiba, Zabibu Kiba aliyofanya juzikati imemtokea puani baada ya kukwaa ugonjwa wa kumlaza kitandani.


 Zabibu alisema kuwa, wageni waalikwa waliohudhuria kwenye bethidei yake walimmwagia maji mengi bila kupumzika ambayo yalimsababishia ugonjwa wa kifua na kwenda hospitali kuchomwa sindano kutokana na maumivu kuwa makali.

“Unajua baada ya kumwagiwa maji vile, usiku sikuweza kulala kabisa kwa sababu nilibanwa na kifua mno, ilibidi niende hospitalini kuchomwa sindano ili kipoe ndiyo nikapata nafuu kidogo,” alisema Zabibu

Post a Comment

 
Top