Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 Rais wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete amemshukuru IGP, Simon Sirro pamoja na Jeshi la Polisi, kwa kuwakamata watu waliokuwa wakilitumia vibaya jina lake pamoja na familia yake kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kupitia mtandao wa Facebook.

Dkt. Kikwete amesema kuwa kuwabainika kwa mtandao huo na kuwakamata ni hatua nzuri hivyo wanahitaji kupongezwa.
“Natoa pongezi nyingi kwa IGP Simon Sirro na Jeshi la polisi@tanpol kwa kuwakamata watu waliokuwa wanatumia vibaya jina langu, la mke wangu Salma na mwanetu Ridhiwani kuwahadaa na kuwaibia Watanzania ninaowapenda sana. Kubainika kwa mtandao huo na kukamatwa ni hatua nzuri ya kupongezwa,” ameandika Dkt. Kikwete katika mtandao wake wa Twitter.

Post a Comment

 
Top