Msanii
wa muziki wa kizazi kipya Dogo Janja ambaye ni mume halali wa muigizaji wa
filamu bongo Irene Pancras Uwoya, ameweka wazi sababu za kupangiwa ratiba na
mke wake huyo, jambo ambalo lilizua kizaa zaa baada ya kuiweka kwenye mtandao.
Dogo Janja amesema alishtuka baada ya kuona ratiba hiyo
imebandikwa ukutani alipoamka, na kueleza sababu zake.
“Nilikuwa
nimelala nimeamka nikakutana na ratiba kwenye ukuta, nikaangalia duh!!
nikaipost insta. Unajua yule ni mshkaji wangu sana alikuwa ananitania, na yeye
ndiye alianza kuipost, na kimvua hiki uniambie ratiba!!? Atadondoka mtu”,
amesema Dogo Janja
Wawili hao
walifunga ndoa ya kimya kimya jambo ambao wengi hawaamni mpaka leo kuwa ni
wanandoa, na pia kutokana na tofauti ambazo wanaonekana wanazo za kiumri.







Post a Comment