Msanii
wa muziki wa kizazi kipya Dogo janja ambaye sasa hivi ameachia video ya wimbo
wake mpya wa 'Wayu wayu' na kuacha gumzo kwa mashabiki kwa kuvaa uhusika wa
mwanamke, na kusema kuwa mke wake ndiye alimfanya awe hivyo.
Janja amesema mke wake ambaye ni muigizaji wa filamu za bongo,
Irene Uwoya, ndiye alianza kumfanyia make up wakiwa mapumzikoni Zanzibar, na
kumvalisha vitu vya kike, ndipo walipopata idea ya kufanya video akiwa kama
mwanamke.
“Mke wangu
kabla sijaanza kushoot alianza kunifanyia make up na kunivesha vesha tulipokuwa
vacation (mapumzikoni) Zanzibar, akawa ananicheka, mpaka siku tunaenda kushoot
ile make up ilibidi anifanyie yeye lakini ilitokea dharula hakuwepo, akaniambia
niende kwa mtu anifanyie make up ya nude mimi hata siijui, hata lile wigi
alinipa mke wangu na mimi nikapita nalo”, amesema Dogo Janja.
Kitendo cha
Dogo Janja kuigiza kama mwanamke kimeonekana kuwakwaza watu wengi wakisema sio
kitu kizuri mwanaume kuvaa hivyo na kujipodoa kama mwanamke, lakini kwa upande
wake amesema ilikuwa ni ubunifu kwa lengo la kuboresha kazi.







Post a Comment