Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Msanii wa nyimbo za Injili nchini Tanzania Emmanuel Mbasha amefunguka na kuwatolea uvivu mabinti wadogo na kusema saizi wengi wao hawaolewi kwa sababu wanawaza starehe na hawafikirii kuhusu maisha zaidi ya starehe zisizo na tija. 

Mbasha amesema kuwa kutokana na hali hiyo ndiyo maana vijana wengi sasa wamekuwa wakioa wanawake wakubwa au ambao wamekomaa kiakili na wanaowaza maisha na si starehe 
"Vijana wa sasa wamefocus na maisha zaidi, hivyo wanahitaji mwanamke aliyekomaa ubongo ambaye wanaweza kufanya mipango ya maisha na kupaa kwa pamoja hadi kwenye ndoto zao. Hii ndiyo inapelekea wanawake wenye umri mkubwa kuolewa kwa kasi kubwa. Hivi vichenchede vinavyowazia kubandika kucha na kope bandia na kusingizia mahusiano ya uongo ili kupata Kiki na mimba hewa sasa havina soko vimebakia kuchuna viinua mgongo vya wanajeshi wastaafu" alisisitiza Mbasha


Post a Comment

 
Top