Familia
ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu imefunguka na kudai kurejea kwa
Mbunge huyo kwa sasa itachukua muda mrefu zaidi tofauti na awali ilivyokuwa
kutokana na upasuaji aliyoufanya siku mbili hizi zilizopita.
Hayo yamebainishwa na msemaji wa familia Alute Mughwai ambaye
pia ni Kaka wa Lissu baada ya kumalizika salama oparesheni wa mguu wake nchini
Ubelgiji ambayo inakuwa ya 19 tokea alipoanza kufanyiwa matibabu tangu
alipopatwa na matatizo.
"Miezi
sita imepita hatusikii lolote kabisa kuhusiana na aliyehusika na tukio la
kupigwa risasi Tundu Lissu au lile gari lililotumika kufanya uhalifu
limepatikana au namna gani? wala bunduki iliyotumika kufyatua zile risasi
hatujapata maelezo yeyote. Hakuna hata senti moja iliyotolewa na Bunge kwaajili
ya gharama za matibabu za Mhe. Mbunge wao Lissu", amesema Mughwai.
Pamoja na hayo,
Alute ameendelea kwa kusema "limejitokeza
tatizo jingine sasa hivi kwamba anahitaji kufanyiwa upasuaji mwingine mdogo ili
kuweza kuipanga mifupa yake vizuri maana yake ni kwamba muda utaenda kidogo
mpaka kurudi kwake nchini Tanzania".
Tundu Lissu
alishambuliwa kwa risasi mnamo Septemba 7, 2017 na watu wasiojulikana akiwa
mjini Dodoma na kisha baadae kupelekwa nchini Kenya kwa matibabu ambapo huko
alifanyiwa oparesheni kadhaa katika mwili wake na mwishowe kupelekwa nchini
Beljium kwa matibabu zaidi ambapo Machi 14, 2018 amefanikiwa kufanyiwa
oparesheni ya 19.







Post a Comment