Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa TFF Michael Richard Wambura ambaye jana amefungiwa maisha kutojihusisha na masuala ya soka, amesema hukumu hiyo imetolewa bila yeye kuhusishwa wakati alionana na Rais kabla ya maamuzi hayo.

Taarifa ya TFF iliyotolewa jana ilieleza kuwa Wambura alibainika na makosa matatu ya kimaadili ikiwemo kugushi nyaraka za Shirikisho pamoja na kupokea fedha kinyume na taratibu vitendo ambavyo vimetafsiriwa kuwa ni kulishushia hadhi Shirikisho hilo.
Baada ya maamuzi hayo Wambura amejitokeza na kuweka wazi kuwa katika huku hiyo hajashirikishwa kwa lolote hata kuitwa kutoa utetezi wake licha ya kukutana na Rais Wallace Karia pamoja na Katibu mkuu siku chache kabla ya kikao cha Kamati ya nidhamu.
Aidha Wambura ameenda mbali zaidi na kusema kuwa kweli amegushi nyaraka za TFF kwanini jeshi la polisi halijahusishwa kwenye uchunguzi wakati ndio chombo chenye mamlaka ya kuthibitisha hilo.
Wambura pia amefafanua kuwa suala hilo limekuja baada ya yeye kuhoji juu ya uhalali wa nafasi mbalimbali ndani ya shirikisho ikiwemo nafasi ya katibu mkuu ambaye anatakiwa kuw awa kuajiriwa lakini kwasasa haiko hivyo.

Post a Comment

 
Top