Jeshi
la Polisi mkoa wa Kipolisi Mara, limetoa taarifa rasmi juu ya kuokotwa kwa
mwili wa mfanya biashara na mmiliki wa mabasi ya Super Sami Samson Josiah ,
ambaye alitoweka na mwili wake kuokotwa mtoni hapo jana.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara Jafari Mohamedi, amesema hapo
jana walipata taarifa kutoka kwa wananchi kuhusu kuokotwa kwa kiroba chenye
mwili ndani, na walipokifungua na kuita watu kutambua, ndipo alipojulikana kuwa
ni mwili wa mfanya biashara huyo anayeishi mkoani Mwanza.
“Jana jioni
tumeweza kupata mwili wa marehemu huyu Samson Josiah ambaye ni mmiliki wa
mabasi ya Super Sammy anayeishi Mwanza, kwamba kuna mwili umeonekana katika mto
ambao unatenganisha mkoa wa Mara na mkoa wa Simiyu unaoelekea mbugani
Serengeti, wananchi waliona kiroba kimefungwa kinaelea, kikavutwa wakajulishwa
polisi kufungua ndani wakakuta mwili wa marehemu, kwa sababu tulikuwa na
taarifa za utafutaji na mashaka juu ya kutoweka kwake, tukajulisha ndugu hao na
wakatambua mwili wa marehemu”, amesema Kamanda Mohamedi.
Kamanda
Mohamedi aliendelea kwa kueleza kwamba marehemu alitoweka kuanzia tarehe
27 mwezi wa pili ambapo aliondoka mkoani mwanza, na ndugu zake walisema kuwa
aliaga anaenda Simiyu kwa shughuli zake za kibiashara na kuna mtu anamdai na
akapotea tangu siku hiyo, na gari yake aliyotoka nayo Mwanza kukutwa imechomwa
mtoto maeneo ya Serengeti mnamo tarehe 8 hadi kuteketea kabisa.
Imeelezwa
kwamba kwa sasa mwili huo umehifadhiwa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara kwa
ajili ya postmoterm, na baadaye utatolewa kwenda kuzikwa, na mpaka sasa watu
wanne wameshikiliwa kufuatia tukio hilo, upelelezi bado unaendelea







Post a Comment