Waziri
wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Harison Mwakyembe amepongeza hatua
ya Baraza la Habari Tanzania, MCT, ya kufungua kesi katika Mahakama ya Afrika
mashariki kupinga Sheria mpya ya Huduma za Habari ya mwaka 2016.
Dk. Mwakyembe amesema, Tanzania ni miongoni mwa nchi 6 Barani
Afrika zilizoridhia mkataba wa kuruhusu wananchi wake kuishtaki serikali katika
Mahakama ya Kimataifa, na kwamba hatua hiyo inaonesha namna ambavyo wananchi
wameanza kutambua namna bora ya kuwasilisha malalamiko yao.
Hivi karibuni
Baraza la Habari Tanzania MCT, lilifungua kesi dhidi ya serikali kupinga Sheria
mpya ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 kwa madai kuwa inanyima uhuru wa vyombo
vya habari.
Awali kabla ya
tamko hilo, Dkt Mwakyembe amekutana na mabalozi wa nchi za Marekani na China
kujadili namna ya kuhifadhi na kuendesha programu ya kumbukumbu za ukombozi wa
bara la Afrika ambayo Tanzania imepewa na nchi za Afrika, kutokana na kuwa
kinara katika kusimamia mapambano dhidi ya wakoloni na uhuru wa nchi za Afrika







Post a Comment