Moja ya Tasnia zinazofanya vizuri na kukamilisha ndoto za watu wengi kupitia vipaji vyao ni Filamu. Mrembo na muigizaji mkongwe nchini Johari, amefunguka juu ya mali anazomiliki zikitokana na kipaji chake cha uigizaji.
Johari amesema filamu imemsaidia kupata mali nyingi ila kikubwa ni kumiliki Kampuni yake.
''Kiukweli nikianza kutaja vitakuwa vingi ila kikubwa nachomiliki ni kitu kinachoniingizia pesa, namiliki kampuni ya RJ, tuko 'share' lakini mimi ni moja ya 'Directors' hivyo ni mmiliki'', alisema Johari.
Vitu vingine ambavyo Johari ametaja kumiliki ni gari pamoja na nyumba huku pia akisisitiza kuwa vipo vitu vingine ni siri kuvitaja kama sehemu ya mafanikio ila amepata vingi kupitia sanaa.
Aidha Johari amewashukuru mashabiki wake kwa mchango wao kupitia sanaa yake kwani umemfanya afanikiwe kuishi vizuri. Johari alianza kufanya vizuri kupitia maigizo na filamu mwanzoni mwa miaka ya 2000.







Post a Comment