Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amevunja kamati ya jumuia ya watumia maji wa vijiji vya Hoza na Salawe huko Mvomero na kuagiza kukamatwa kwa viongozi wa jumuia hizo baada ya kubaini kushindwa kusimamia uendeshwaji wa mradi
Mh. Aweso amefikia uamuzi huo baada ya wakazi wa kata hiyo wakiongozwa na Mbunge wa jimbo la Mvomero Murad Sadiq kudai licha ya malengo ya serikali kutaka kuwaondolea shida ya maji katika kata hiyo changamoto ni viongozi hao kushindwa kusimamia fedha za michango ya wananchi.
Maradi huo wa maji unaotekelezwa katika vijiji vya Hoza na Salawe mpaka sasa umetumia shilingi milioni 503 huku utekelezwaji wake ukidaiwa kuwa chini ya kiwango, kutokana na kuwepo miundombinu chakavu jambo ambalo Naibu Waziri hakuridhishwa nalo.
Imedaiwa kuwa katika mradi huo viongozi wamefanya ubadhilifu wa zaidi ya shilingi million 6 zilizotokana na michango ya wananchi katika kuendeleza mradi huo.






Post a Comment