Menu

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye ni mkongwe kwenye game na aneendelea kukimbiza, Judith Wambura au Jaydee, ametoa sababu ya kuandika wimbo wake mpya wa 'Anaweza' ambao amemshirikisha msanii wa Jamaica Luciano.

Jaydee amesema vijana wengi sasa hivi wamekata tamaa na maisha kutokana na mambo mbali mbali yanayowakabili, hivyo akaona ni vyema iwapo atatunga kitu cha kuweza kuwafariji.
“Vijana wengi sana kwa kipindi hiki wameonakana kukata taa, na kuna vitu vingi ambavyo wanapitia, mambo mengi yamekuwa kelee, party, fake life, nimefikiri ni muda muafaka kuwapa moyo watu ambao wamekata tamaa kuwaambia kuwa wanaweza”, amesema Lady Jaydee.
Kazi hiyo mpya ya Jaydee audio imetengenzwa na mpezni wake Spice huku video ikitengenzwa na Justine Campos wa  Afrika Kusini.
 

Post a Comment

 
Top